Taaluma na Matokeo

Tunajivunia ubora wa elimu na ufaulu wa hali ya juu unaowafanya wanafunzi wetu kung'ara kitaifa.

📚 MTAALA WETU 📚

Masomo Yanayofundishwa

Tunatoa elimu inayofuata mtaala wa Taifa (NECTA) huku tukisisitiza uelewa wa kina kwenye masomo ya Sayansi, Biashara, na Sanaa.

📖 O-Level (Kidato cha I - IV)

Wanafunzi wanajengewa msingi imara kupitia masomo ya lazima na ya kuchagua kulingana na vipaji vyao.

  • Fizikia (Physics)
  • Kemia (Chemistry)
  • Biolojia (Biology)
  • Hisabati (Basic Math)
  • Jiografia (Geography)
  • Historia (History)
  • Kiingereza (English)
  • Kiswahili
  • Uraia (Civics)
  • Biashara (Commerce)
  • Uhasibu (Book Keeping)

🎓 A-Level (Kidato cha V - VI)

Tunatoa michepuo (combinations) inayoandaa wanafunzi kuwa wataalamu mahiri katika vyuo vikuu.

  • PCB (Physics, Chem, Bio)
  • PCM (Physics, Chem, Math)
  • CBG (Chem, Bio, Geog)
  • EGM (Econ, Geog, Math)
  • HGL (Hist, Geog, Lang)
  • HGK (Hist, Geog, Kisw)
  • HKL (Hist, Kisw, Lang)
  • General Studies (GS)
  • BAM (Basic Applied Math)
🏆 REKODI ZETU 🏆

Matokeo na Mafanikio

Kila mwaka, wanafunzi wetu wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye mitihani ya Taifa na kutuletea heshima kubwa.

Cheti cha Mshindi wa Kwanza Fizikia Taifa 2024

Fahari Yetu: Aron Weisy Wikedzi

Historia iliandikwa mwaka 2024 pale mwanafunzi wetu, Aron Weisy Wikedzi, alipoibuka Mshindi wa Kwanza Kitaifa katika somo la Fizikia (CSEE 2024).

Kutokana na umahiri huo, alitunukiwa cheti maalum na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Hii ni dhihirisho la ubora wa walimu wetu wa sayansi, uwepo wa maabara za kisasa, na juhudi za wanafunzi wetu.

#1

Kitaifa Fizikia '24

100%

Ufaulu wa Daraja I - III